RAIS WA KOREA KUSINI: KUNA UWEZEKANO MKUBWA WA VITA NA KOREA KASKAZINI MAENEO YA MPAKANI.

Bofya Hapa

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In ameonya kwamba kuna “uwezekano mkubwa” wa kutokea mapigano ya kijeshi mpakani mwake na Korea Kaskazini wakati mvutano kuhusu matarajio ya Pyongyang kuhusu nyuklia ukiongezeka.

Moon aliyeapishwa wiki iliyopita ameonya kwamba mpango wa Korea kaskazini wa nyuklia na maroketi  umekuwa “ukishika kasi”, siku chache baada ya Pyongyang ilipoanzisha kile kinachonekana kuwa kombora la masafa marefu .

“Jeshi letu limedumisha utayari wa kijeshi ambao hautaruhusu uchokozi wa aina yoyote na tunayo dhamira na uwezo pindi ukihitajika mara moja na kuadhibu kwa nguvu, hata kama adui zetu wataleta chokochoko za silaha. Kama rais, nitaendeleza zaidi uwezo huo,” alisema rais huyo.

Mvutano baina ya Washington na Pyongyang  umezidi kushika kasi katika wiki za hivi karibuni kutokana na utawala wa Trump kusema kwamba hatua za kijeshi zilikuwa ni njia mbadala inayozingatiwa na Korea kaskazini yenyewe ikitishia kulipiza kisasi kikubwa.

Rais Moon ambaye ana siasa za mrengo wa kushoto anapendelea ushiriki wa Korea kaskazini katika meza ya majadiliano lakini baada ya uzinduzi wa kombora siku ya Jumapili, kiongozi huyo amesema mazungumzo yatawezekana “ikiwa Pyongyang itabadili tabia yake”.