RC MAKONDA AWEKA UTARATIBU WA KUWAHUDUMIA WALIOFANYIWA UPASUAJI NDANI YA MELI

Bofya Hapa


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.PAUL MAKONDA amesema Serikali inaweka utaratibu wa kuendelea kuwahudumia Wagonjwa waliotibiwa ndani ya Meli ya Jeshi la China pindi Meli hiyo itakapoondoka wakiwemo wale waliofanyiwa Upasuaji na kuonekana wanahitajika kuendelea kupewa Matibabu hadi hapo watakapopona.

RC MAKONDA amesema kundi la Pili litakalohudumiwa ni Wale waliopatiwa matibabu lakini kuna Dawa watatakiwa kuendelea kuzipata Serikali itaweka utaratibu wa kuendelea kutoa Dawa hizo Bure hadi wapone.

Aidha RC MAKONDA amesema watu wote waliopatiwa Namba za Matibabu watahudumiwa pasipo usumbufu wowote.

Amesema idadi kubwa ya watu waliojitokeza kupima Afya haimaanishi kwamba Watanzania ni wagonjwa Bali ni mwitikio wa watu kutoka mikoani na nje ya Nchi waliofuata huduma hiyo.

Lengo la Serikali kutoa huduma ya Matibabu Bure ni kuwawezesha wasiokuwa na kipato kuweza kupata matibabu ili kuhakikisha Hakuna mwananchi anaepoteza maisha kwa kigezo cha kutomudu gharama za matibabu.

Ameishukuru Serikali ya China kwa upendo walioonyesha kwa Wagonjwa waliokwenda kutibiwa Bure Hali inayodhihirisha Ukomavu wa Mahusiano baina ya Tanzania na China.