REAL MADRID WATOKA SARE NA ATLETICO MADRID,RONALDO NA GRIEZMANN WATUPIA

Bofya Hapa

Pamoja na kuwa vilabu vya Real Madrid na Atletico Madrid kuwa havina nafasi katika mbio za kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu Hispania msimu huu kutokana na kasi ya mpinzani wao mkuu wa FC Barcelona, mchezo wa Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid bado ulikuwa na mvuto wa kipekee leo.

Leo April 8 2018 katika uwanja wa Santiago Bernabeu Real Madrid waliwakaribisha wapinzani wao wa jadi kutoka jiji moja la Madrid club ya Atletico Madrid, nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ameendeleza kuonesha umahiri wake kama ilivyokuwa kwa Antoine Griezmann wa Atletico Madrid.

Real Madrid wakiwa nyumbani walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 54 kupitia kwa staa wao Cristiano Ronaldo ila furaha yao ilidumu kwa dakika zisizozidi mbili kwani dakika ya 57 Antoine Griezmann aliisawazishia Atletico Madrid na kuufanya mchezo umalizike kwa kufungana sare ya 1-1. Matokeo hayo yanazidi kumuweka pazuri zaidi mpinzani wao mkuu

FC Barcelona ambaye baada ya matokeo hayo atakuwa anaongoza Ligi kwa tofauti ya point 11 dhidi ya Atletico Madrid anayemfuatia kwa kuwa na jumla ya point 68 wakati Real Madrid wakiendelea kusalia nafasi ya tatu kwa kuwa na jumla ya point 64.