RUGE AIBUKIA KWA VIJANA TENA,AWAPA SIRI YA MCHEZO

Bofya Hapa

Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amewataka vijana nchini wasisubiri kushindwa maisha kwingine ndio waingie kwenye ujasiriamali. Ruge alitoa kauli hiyo jana wakatia akizungumza na vijana katika kongamano la kujadili masuala ya ujasiriamali lililoandaliwa na kituo cha biashara cha chuo kikuu cha Dar es Salaama (UDIEC). ”

Nadhani ifike mahala ujasiriamali uanzie ndani ya familia zetu siyo tusubiri mpaka kushindwa maisha sehemu nyingine, maana hiyo haiwezi kukusaidia kwa sababu utakuwa unafanya kitu ambacho hakipo moyoni mwako,” alisema Ruge. Alisema licha ya vijana wengi kulalamikia suala la kutokuwa na mitaala yenye kuelekeza wanafunzi kujiajiri wenyewe bado yeye anaamini suala la kujiajiri linapaswa kuanzia ndani ya mtu mwenyewe na siyo kufundishwa. “

Haiwezekani kijana mwenye nguvu zake unalala saa 12, unasubiri uambiwe kazi ya kufanya na wala hujiangaishi kuwa mbunifu, na ndio maana Serikali yenyewe ilitoka kwenye mfumo wa ujamaa na kwenda kwenye ubepari ili kila mmoja aweze kuwa huru kivyake,” Alisema Ruge.

Awali Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge, Ajira, Walemavu) Stella Ikupa alisema Serikali itaendelea kuwajengea vijana mazingira mazuri ya ufanyaji wa biashara.