SASHA ALILIA PICHA ZA NUSU UTUPU MTANDAONI

Bofya Hapa

MUUZA nyago machachari Bongo, Sasha Kassim amesema kitendo cha Naibu Waziri wa Habari Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kulivalia njuga suala la picha za utupu mtandaoni linamtesa mno kisaikolojia hadi kufikia hatua ya kulia kwani picha hizo zimembadilisha kimaisha. Akizungumza na Mikito Nusunusu, Sasha alisema kuwa jambo hilo limemuumiza mno kwani moja ya sababu inayomtesa na kumuathiri kisaikolojia ni kwamba, picha hizo zimempa madili mengi ya kumuingizia pesa ikiwemo matangazo ya biashara. Naumia mno, picha nilizokuwa napiga kwanza ni starehe yangu, lakini pia zimebadilisha maisha yangu kutokana na dili mbalimbali nilizokuwa napata, zimenipa dili za kazi, zikanipa mchumba na pia zimenipa umaarufu mtandaoni na kwenye jamii kwa kiasi chake, hata hivyo siwezi kushindana na serikali nitapunguza kidogo, vinginevyo nitayumba kimaisha,” alisema.