SHILOLE KIUNO ADAI SITOACHANA NA UCHEBE WANGU LEO WALA KESHO

Bofya Hapa

                    BAADA ya habari kusambaa kwamba ana mgogoro na anamtesa mchumba wake, Uchebe, staa wa muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameibuka na kusema hataachana naye leo wala kesho. Akifungukia taarifa hizo za kwenye mitandao ya kijamii,

 

Shilole alisema kuwa, taarifa hizo siyo za kweli na yeye na mchumba wake wako sawa na wanaendelea na mahaba yao kama kawaida hivyo wanaowatakia mabaya ili waachane, wakajipange.

 

Nashangaa sana maana mchumba wangu hana akaunti Instagram ila kuna watu wanafungua akaunti feki na kuandika mambo ya ajabu ambayo hayapo kabisa, niwaambie tu hatuachani ng’o tuko tunaendelea na mahaba yetu kama kawa,” alisema Shilole.