STAA SHILOLE ATAJA RASMI SIKU YA NDOA YAKE

Bofya Hapa

HATIMAYE mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameibuka na kutangaza rasmi tarehe ya ndoa yake na mchumba wake, Uchebe ikiwa ni baada ya mashabiki kusubiri kwa hamu.

Akichonga na Mikito Nusunusu, Shilole alisema anatarajia kuolewa Desemba 20, mwaka huu na harusi yake itakuwa babu kubwa kwani amejipanga.

Alipobanwa kuwa anaolewa kwa sababu amepewa ujauzito alikana kuwa siyo mjamzito na kusisitiza kuwa ukweli wote utaonekana siku ya harusi yake.

“Kama nina ujauzito mbona haufichiki ni siku chache tu zimebaki kuelekea terehe ya ndoa yangu kila anayehisi nina ujauzito aje ahudhurie atagundua hilo, hapa nimenenepa tu,” alisema Shilole.