Uongozi wa Yanga wafikia maamuzi haya juu ya ‘Donald Ngoma’

Bofya Hapa

Uongozi wa Klabu ya Yanga SC umefikia maamuzi ya kukaa chini na mshambuliaji wao, Donald Ngoma na kujadili vitendo vyake vya utovu wa nidhamu ndani ya timu hiyo. Ngoma mwenye misimu miwili Jangwani, amekumbwa na kashfa za kuondoka na kugomea kuichezea timu hiyo kwa kisingizio cha kuwa majeruhi msimu huu na kuwa na msaada kidogo ndani ya timu hiyo kutokana na kutocheza mara kwa mara kwa sababu ya majeraha ya goti ambalo limemfanya akose michezo mingi ya timu hiyo.
Uongozi wa Yanga SC kupitia kwa Katibu wa Klabu hiyo, Boniface Mkwasa amesema wataongea kwa kina na mshambuliaji huyo juu ya safari yake ya Afrika Kusini alipokwenda kutibiwa na kuzidisha siku.