WEMA SEPETU NA ZARI THE BOSS LADY KUMEKUCHA,HAPATOSHI,DJ WA DIAMOND JORMY JONES AFANYA YAKE

Bofya Hapa

Wema, Zari Hapatoshi Mitandaoni, Maua Yazua Gumzo Balaa! Siku chache baada ya mzazi mwenza wa Mbongo Fleva, Diamond Platnumz, Mwanamama Zari The Boss Lady, kupost picha ya ua jeusi katika ukurasa wake wa Instagram, akiashiria kupigana kibuti na mzazi mwenziye huyo.

Queen wa Bongo Muvi, Wema Sepetu, ambaye hivi karibuni ameibua minongo’no kuwa amerudiana na x- wake ambaye ni mzazi mwenza wa Zari, Diamond, ambapo leo amewashangaza mashabiki mitandaoni kwa kuposti picha ya Ua jekundu kwenye ukurasa wake wa Instagram, linaloashiria Mapenzi ya dhati, na kuwaachama mashabiki njia panda wasijue kuwa ua hilo ni kijembe cha kumuonyeshea Zari kuwa ni kweli amerudiana na mbongo Fleva huyo au lah!

Baada ya posti hiyo ya Wema, .mashabiki wamekuwa na maoni tofauti tofauti, huku wengine wakidai hakutakiwa kupost ua hilo, wengine wamempongeza na kuonyesha kutamani kuona wawili hao wakirudiana.