WEMA SEPETU,JACKY WOLPER ,AUNT EZEKEL NA KAJALA,NI MASTAA BONGO,GUSA UPOTEE

Bofya Hapa

PENYE wengi pana mengi. Kila uchwao katika ulimwengu wa mastaa kuna mengi yanayotokea yakiwemo mazuri na mabaya, ya kufurahisha na kuhuzunisha.
Wapo baadhi ya mastaa hasa wa kike ambao wanapoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na wanaume au ndoa, wahusika hujikuta wakiishia pabaya ambapo gumzo hubaki kwamba wasanii hao ni gusa upotee na hii ni kutokana na wengi wanaojihusisha nao hujikuta wakipotea. Yaani kama walikuwa na fedha, hufilisika au maarufu umaarufu wao hupotea ghafla huku wengine wakiishia jela.
WEMA SEPETU
Mwanadada huyu ambaye ni staa wa filamu za Kibongo amewahi kuwa na uhusiano na wanaume tofautitofauti ambapo miezi kadhaa iliyopita aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanaume aliyesemekana kuwa ni mume wa mtu aliyejulikana kwa jina la Bakari Kila.
Wawili hawa walidumu kwenye uhusiano kwa muda mfupi mno na ghafla mwanaume huyo alinaswa kwa msala wa madawa ya kulevya nchini Kenya na kuswekwa lupango kabla ya kupotea jumlajumla.
KAJALA MASANJA
Mkali huyu wa filamu za Kibongo anaingia kwenye listi ya mastaa wa kike ambao ni gusa upotee kutokana na mumewe, Faraji Agustino kukutwa na mkasa wa kutakatisha pesa na kufungwa, lakini mwaka jana aliachiwa huru baada ya kushinda rufaa.
Mume wa Kajala alipata matatizo hayo muda mfupi tu baada ya kuingia kwenye ndoa na staa huyo kwani hawakuwa wamebahatika kupata mtoto na hata baada ya kutoka jela, kwa sasa hajulikani alipo na Kajala anaendelea na maisha yake kama kawaida akiwa hajaolewa.

JACQUELINE WOLPER
Staa huyu wa filamu za Kibongo ana kismati cha kupata wapenzi, lakini hadumu nao huku wengine wakimvisha pete za uchumba na baadaye huishia kusikojulikana.
Wolper alitikisa mno alipokuwa kwenye uhusiano na Abdallah Mtoro ‘Dallas’ ambaye alikuwa mfanyabiashara mwenye pesa chafu. Ilisemekana kwamba baada ya Dallas kuwa kwenye uhusiano na Wolper alidaiwa kufulia kabla ya kuwa kimya hadi sasa ikielezwa kwamba amekuwa mtu wa dini (Uislam) mno.

LULU SEMAGONGO ‘AUNTY LULU’
Mwigizaji huyu wa Bongo Movies ambaye pia ni mtangazaji wa runingani asiyekuwa na kituo, aliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji mwenzake, Bond Suleiman, lakini baadaye walimwagana.
Wakati Bond akiwa na Aunty Lulu alikuwa ni mtangazaji wa Kipindi cha Action and Cut cha Channel Ten, lakini kwa sasa amepotea na kwa mujibu wake ni kwamba analima mananasi huko Chalinze vijijini na hajihusishi tena na masuala ya sanaa.

BABY MADAHA
Msanii huyu wa Bongo Fleva na Bongo Movies, miaka kadhaa iliyopita alikuwa na meneja wake ambaye ni raia wa Kenya aliyejulikana kwa jina la Joe Kariuki.
Walifanya kazi pamoja kwa mwaka mmoja ambapo walijikuta wakiingia kwenye uhusiano wa kimapenzi, lakini baadaye walimwagana na hadi sasa mwanaume huyo amepotea na hajawahi kumsimamia msanii mwingine kwa hapa Bongo, yupo kwao huko Kenya.

ISABELA MPANDA ‘BELLA’
Mwanamama huyu ni msanii wa muziki na filamu ambaye amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki, Luteni Kalama ambaye alitua kwa Bella baada ya kuvunjika kwa ndoa yake.
Penzi lao lilidumu kwa miaka mingi, lakini walikuja kumwagana na kila mmoja kwa sasa ana maisha yake huku Bella akiwa na mwanaume mwingine. Kwa upande wa Kalama hajulikani yuko wapi kwani hata kimuziki hasikiki tena.

AUNT EZEKIEL
Staa huyu wa filamu alikuwa ni mke wa ndoa wa mfanyabiashara Sunday Demonte ambaye makazi yake ni Dubai.
Ni kama gundu kwani baada ya kuingia kwenye ndoa na Aunt, Demonte alipata matatizo ya kufungwa jela na hadi sasa haijulikani kama ametoka au bado ila mwanamama huyo yupo na maisha yake mengine na ana mwanaume mwingine ambaye ni densa wa WCB, Moze Iyobo na tayari wamejaliwa mtoto mmoja wa kike aitwaye Cookie.
RIYAMA ALLY
Mwanamama huyu anaingia kwenye orodha hii baada ya kufunga ndoa na msanii wa Bongo Fleva, Leo Mysterio wakati huo akiwa ameshaanza kujulikana kwa mashabiki wake.
Tangu waingie kwenye ndoa, Riyama ni kama amempoteza mumewe huyo kwani hata kwenye anga la muziki hasikiki tena na watu wamemsahau kabisa.

Risasi Vibes