YANGA WAKUTANA NA MISHAHARA TAIFA

Bofya Hapa

WACHEZAJI wa Yanga juzi jioni mara baada ya mechi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, akaunti zao za benki zilinona baada ya uongozi wa timu hiyo kuwalipa mishahara yao. Hiyo ikiwa ni siku chache tangu wakae kikao na viongozi wa timu wakihoji lini watalipwa mishahara yao na wataishije kwenye kipindi hiki kigumu ambacho mashabiki wanawapa presha wakidai matokeo.

Yanga inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 43 huku Simba ikiongoza na 46. Spoti Xtra ilishuhudia Wachezaji wengi wakinong’onezana kwenye korido za Taifa kwamba mzigo umeingia wakaondoka na sura za tabasamu. Habari za uhakika ambazo Spoti Xtra imezipata ni kwamba wamelipwa mshahara wa mwezi mmoja bado miezi miwili pekee ambayo uongozi umewaahidi kwenye vikao vya ndani kwamba wanapambana na watalipa ndani ya muda mfupi.

Mmoja wa viongozi wa Yanga alidai suala hilo ni siri za ndani lakini lengo lao la kuwalipa ni kutaka wapambane kwa moyo kwenye mechi ya Stand United kesho Jumatatu ndani ya Uwanja wa Taifa kabla kuondoka Jumanne kwenda Botswana. Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alipoulizwa kuhusiana na hilo aliishia kucheka tu. STORI NA WILBERT MOLANDI