ZARI THE BOSS LADY MAPYA TENA: YASEMEKANA AMUACHA HAMISA AOLEWE,MAZITO YAIBUKA

Bofya Hapa

              Pamoja na kwamba, mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa hadharani, mbele za watu au akihojiwa na vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii anakanusha uhusiano wake na mzazi mwenzake ambaye ni msanii wa Bongo Fleva kuvunjika, nyuma ya pazia akiwa na watu wake wa karibu anaeleza ukweli kwamba, hakuna mapenzi tena kati yao.

 

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya kuaminika, hivyo ndivyo ilivyo kwa mwanaume huyo ambaye naye akiwa mbele ya ‘kamera’ anadai kuwa, wapo vizuri tu, lakini habari za uhakika ni kwamba ‘nyumba’ imewaka moto. Habari zilizo kwenye makabrasha ya Ijumaa Wikienda, zinadai kuwa, Zari anaendelea kutikisa mitandao ya kijamii na ameamua kumuachia mzazi mwenzake huyo kwa mwanamitindo matata wa Bongo, Hamisa Hassan Mobeto ili aolewe naye baada ya kuzaa naye mtoto wa kiume, Abdul Naseeb ‘Prince Dully’ au Dylan.

SABABU YA YOTE Ilidaiwa kwamba, sababu ya hayo yote hadi Zari kufi kia hatua ya ‘kususa’ ni kufuatia skendo hiyo ya mwanaume wake huyo kuzaa na Hamisa kuendelea kushika kasi kila kukicha. Chanzo kimojawapo cha Ijumaa Wikienda kilidai kwamba, Zari, baada ya kuona ‘vurugu’ zimekuwa ni nyingi kuhusiana na mzazi mwenzake huyo aliyezaa naye watoto wawili, ameamua kujiweka pembeni ili kuondoa msongamano, japokuwa jambo hilo hataki kulionesha hadharani.

 

UBUYU WA MTU WA KARIBU Chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa Zari aliyeko Bongo alimwaga ubuyu kuwa, mwanamama huyo amefi kia hatua ya ‘kuuchoka’ uhusiano huo kwani mwanaume wake huyo amekuwa akimuumiza kwa kusaliti penzi lao mara kwa mara hivyo kumshushia heshima. Kilidai kwamba, katika mazingira hayo ambayo mwanaume huyo amekuwa akionywa, lakini hasikii, safari hii Zari ameamua kumsihi aendelee na Hamisa kwa sababu tayari ameshazaa naye. “Yaani sasa hivi Zari ndiyo ameamua kabisa, kama mbwai mbwai tu! Amemuomba mzazi mwenzake huyo aendelee na Hamisa kiroho safi kabisa!

 

Na pia akasema, ameamua kumuachia Hamisa aolewe na baba huyo wa mtoto wake kuliko kuendelea kupata fedheha za kuwa na uhusiano na wanawake tofauti na tena wasichana wadogo ambao siyo levo zake (Zari),” kilifunguka chanzo hicho na kuongeza: “Kama ni kuchoka, kiukweli Zari yupo nyang’anyang’a hadi ameamua kunyoosha mikono.” ZARI AANZA MAISHA MAPYA Mpashaji wetu huyo aliendelea kusema kuwa, kwa sasa Zari ameamua kuanza maisha yake mapya bila baba watoto wake huyo huku akiamua kumfanya Hamisa kuwa mmoja wa marafi ki zake kwa kuwa ana mtoto ambaye ni damu moja na watoto wake (Tiffah na Nilan).

 

AANZA ‘KU-LIKE’ PICHA ZA HAMISA Chanzo hicho kilidai kuwa, ndiyo maana mara nyingi Zari anatembelea ukurasa wa Instagram wa Hamisa na ‘ku-like’ picha zake kuonesha kuwa amemuachia kiroho safi . “Sasa hivi Zari ameamua kuwa pamoja na Hamisa, kuhakikisha anapata haki za mtoto wake huku yeye akiwa anaendelea na maisha yake mengine kabisa, bila mzazi mwenzake huyo. “Huwezi kuamini, lakini Zari amefi kia hatua ya kumsihi baba watoto wake huyo afunge ndoa na Hamisa kuliko kuendelea kurukaruka hovyo,” alisema mpashaji huyo na kuongeza:

 

Yaani yeye amesema ishu ya kulea watoto wala haimpi shida kwani hata kabla ya kuzaa na msanii huyo alikuwa anawalea vizuri tu watoto watatu aliozaa na Ivan (aliyekuwa mumewe).” Alipotafutwa Hamisa hakuwa tayari kuzungumzia uhusiano wa wawili hao kwani tayari ameshaanza mapambano ya kutafuta haki yake baada ya kutelekezwa na mwanaume huyo.

 

YALIYOJIRI WIKIENDI Katika kuonesha kuwa hali inazidi kuwa mbaya kati ya Zari na baba watoto wake huyo, mbali na zoezi la kufutiana picha zao kwenye kurasa za Instagram, pia suala la mwanamama huyo kutomtakia jamaa huyo heri ya siku ya kuzaliwa nalo liliendelea kuzua gumzo. Mbali na hilo, pia kuna ishu mpya ambapo mwanaume huyo alitangaza kuwa kwenye shoo yake ya jijini Kampala nchini Uganda, wikiendi iliyopita angeambatana na Zari, lakini tofauti na matarajio ya wengi, mwanamama huyo alikanusha jambo hilo hivyo kuzidisha ‘mtiti’ baina yao